IRAN: SANAMU ZAFUNIKWA UCHI RAISI APITE...
Sanamu zinaoonyesha uchi nchini Italia zilifunikwa wakati wa ziara ya Rais wa Iran Hassan Rouhani nchini humo.
Sanamu hizo zilifunikwa Jumanne kuzuia kumuudhi kiongozi huyo wa Iran, taifa mabalo hufuata sheria kali za Kiislamu.
Maafisa wa Italia pia hawakuwaandalia wageni ndivai kama ilivyo kawaida.
Iran, ambayo ni Jamhuri ya Kiislamu, ina sheria kali za kudhibiti unywaji wa pombe.
Bw Rouhani alikutana na Waziri Mkuu wa Italia Matteo Renzi na baadaye akatoa hotuba katika makavazi ya Capitoline, mjini Roma baada ya kutia saini mikataba na kampuni za Italia Jumatatu.
Baadaye Jumanne, kiongozi huyo alikutana kwa takriban dakika 40 na kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis.
Bw Rouhani alimuomba Papa Francis amuombee na pia akampa zawadi ya zulia.
Kiongozi huyo wa Iran yumo kwenye ziara ya siku tano barani Ulaya.
Ufaransa, taifa ambalo kiongozi huyo alitembelea Jumatano, limesema halitakosa kuwaandalia wageni divai kama walivyofanya maafisa Italia.
Bw Rouhani amenukuliwa Jumatano na shirika la habari la AFP akisema hakuwaagiza maafisa wa Italia wafunike sanamu hizo.
"Najua Wataliano ni wakarimu sana, na hutaka sana kuwafurahisha wageni wao na nawashukuru kwa hilo,” ameongeza.
Bw Rouhani hukataa kuhudhuria hafla ambazo watu hunywa pombe, bia au mvinyo huandaliwa, na vileo hivyo havikuandaliwa wakati wa chakula cha mchana na Rais Sergio Mattarella na pia maakuli ya jioni na Renz.
Maafisa wao hata hivyo wanajikuna vichwa kutokana na tamko la Ufaransa kwamba haitatii hilo.
No comments
+255716829257