Habari mpya

AL-SHABAB KUWAZUILIA WAKENYA.

Image copyrightAP
Image captionwapiganaji wa Alshabaab
Kundi la wapiganji wa al-Shabab limesema kuwa linawazuilia 'wafungwa wa kivita' kutoka Kenya kufuatia shambulio lao katika kambi ya kijeshi kusini mwa Somalia.
Al-Shabab, ambao waliivamia kambi hiyo, wamesema kuwa wanajeshi 100 wanaohudumu katika muungano wa Afrika waliuawa.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema siku ya Ijumaa kwamba baadhi ya wanajeshi wa Kenya waliuawa lakini hakutoa idadi yao.
Al Shabaab wamesema kuwa ni mara ya kwanza kwa kikosi chake cha Saleh Ali Saleh Nabhan kutekeleza shambulio ndani ya Somalia.
Image copyrightAFP
Image captionRais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Mashambulizi yake mengine yamekuwa nchini Uganda na Kenya.
Saleh Ali Saleh Nabhan alikuwa kiongozi wa kundi la al Qaeda katika eneo la Afrika mashariki ambaye aliuawa katika shambulio la Marekani nchini Somalia mwaka 2009.

No comments

+255716829257