Habari mpya

Rapper Nipsey Hussle afariki dunia

Inaripotiwa kuwa Rapper Nipsey Hussle’33 kutokea nchini Marekani amepigwa risasi na kufariki asubuhi ya kuamkia leo April 1,2019 jijini Los Angeles, inaelezwa kuwa alipigwa risasi akiwa nje ya duka lake la nguo ambapo mpaka sasa watu wawili wanaripotiwa kujeruhiwa.
Pia taarifa nyingine zinadai kuwa kabla ya Nipsey  kupoteza maisha aliwahi kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba  “Kuwa na maadui ni baraka”, ikiwa taarifa za kifo chake zinahusishwa na maadui aliokuwa nao.
Rapper Nipsey ameacha mke ambaye ni muigizaji wa Hollywood anayefahamika kwa jina Lauren London na ameacha jumla ya watoto wawili Kross Asghedom, Emani Asghedom.

No comments

+255716829257