Habari mpya

Rapper DMX aandamwa na madeni, anatarajia kuuza nyumba yake

Inaripotiwa kuwa Rapper DMX ameamua kuweka sokoni nyumba yake aliyoinunua mwaka 2000 yenye thamani ya kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 1 za Kitanzania ($649,000) na aliipata alipokuwa akifanya vizuri kwenye game ya muziki wa Hip Hop.
Inaelezwa kuwa nyumba hiyo ambayo ipo Mount Kisco mjini New York itauzwa kwa bei ya punguzo hadi kufikia kuuzwa shilingi Bilioni 1.6 za Kitanzania ($699,000) na inatajwa kuwa rapper huyo anadaiwa zaidi ya shilingi Bilioni 3 za Kitanzania. Rapper DMXanajaribu kulipa madeni yake baada ya kukaa jela kwa mwaka mmoja kutokana na kosa la ukwepaji kodi.
DMX aliachiwa huru January 2019 baada ya kukaa jela miezi 12 kwa kukutwa na hatia ya ukwepaji kodi na kudaiwa kiasi cha zaidi ya dola milioni 1.7, sasa moja ya masharti ya kuachiwa yalikuwa ni lazima alipe kiasi hicho cha pesa.

No comments

+255716829257