Habari mpya

SUMATRA YATOA RUHUSA KWA MAGARI MADOGO KUSAFIRISHA ABIRIA MIKOANI


Inaelezwa kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imepanga kusajili magari zaidi, yakiwamo mabasi madogo, kwa ajili kusafirisha abiria katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Sumatra, Bw.Johanes Kahatano, ambapo anadai kuwa lengo ni kuhakikisha wanatatua changamoto ya usafiri na adha ambayo wananchi huipata wakati wa kusafiri katika kipindi cha mwisho wa mwaka.
-
Aidha aliongeza kuwa magari yatakayosajiliwa ni yale yenye ubora na yenye uwezo wa kubeba angalau kuanzia abiria 30.

No comments

+255716829257