Habari mpya

Ijue sheria ya ujenzi karibu na fukwe za bahari, kingo za mito na maziwa

Mwanasheria wa kujitegemea, Leonard Manyama amezungumzia sheria kuhusu uendeshaji wa shughuli ama kufanya ujenzi ndani ya mita 60 za fukwe za Bahari, kingo za Mito ama Ziwa.
Wakili Manyama amesema suala la ulinzi na usimamizi wa mazingira linasimamiwa na sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004, ambapo kifungu cha 157 kinaeleza wazi ni marufuku kwa mtu yoyote kuendesha shughuli yoyote ambayo inaathiri utunzaji wa mazingira ndani ya mita 60 kutoka ndani ya bahari, mito ama ziwa.
Amesema fukwe za bahari zinalindwa kwa mujibu wa sheria hiyo ambapo inatamkwa fukwe hizo za bahari kuwa ni maeneo ambayo yanatumika kwa ajili ya matumizi ya umma, ambapo mtu yoyote haruhusiwi kufanya shughuli itakayoathiri maeneo hayo.
“Ni kosa la jinai kujenga katika fukwe bila kuwa na kibali ama kuzuia njia kwani hilo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria na mtu akibainika adhabu yake ni faini ya Shilingi Milioni 10 ama kifungo jela,”amesema.

No comments

+255716829257