Habari mpya

Yanga imeendeleza rekodi ya kutopoteza msimu huu

Club ya Dar es Salaam Young Afrcans (Yanga) imeendeleza rekodi yake chanya ya kutopoteza katika game zake za Ligi Kuu Msimu huu wa 2018/2019 baada ya kuikaribisha Lipuli FC kucheza game yake ya tisa ya Ligi Kuu.
Yanga imeikaribisha Lipuli FC na imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0, goli la Yanga limefungwa na Herieter Makambo dakika ya 10 baada ya kutumia vyema pasi ya Mrisho Khalfan Ngassa iliyoshindwa kuzuiliwa na mabeki wa  Lipuli FC, Yanga hadi sasa ndio pekee Ligi Kuu ambayo haijapoteza mchezo msimu huu.
Ushindi huo unazidi kuiweka pazuri Yanga SC ambayo imecheza game yake ya tisa ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu pasipo kupoteza mchezo, ambapo sasa ipo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point 25 nyuma ya Azam FC wanaoongoza Ligi kwa point 27 wakiizidi Yanga michezo miwili

No comments

+255716829257