Habari mpya

Watu 131 wathibitishwa kufa hadi sasa ajali ya kivuko cha MV Nyerere

Rais John Magufuli amehutubia waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa kufikia sasa imethibitika kwamba miili ya watu 131 imeopolewa na bado kuna hofu kwamba wengine wengi hawajapatikana.
Ameeleza kuwa rasmi kivuko hicho cha MV Nyerere kina uwezo wa kubeba abiria 101, lakini kwa takwimu zilizopo sasa zinazojumuisha miili iliyopatikana pamoja na manusura, ni wazi kwamba chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria kupita kiasi.
Rais Magufuli ameagiza bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti.
Ameagiza wote waliohusika na mkasa huo wakamatwe akiwemo kapteni wa kivuko hicho, ambaye taarifa zilizopo, tayari amekamatwa kusaidia katika upelelezi. Kadhalika ameagiza kuundwa kwa timu itakayoshughulika na uchunguzi huo.
Amewataka wanasiasa kutotumia mkasa huu kama 'kiki za kisiasa' na waache vyombo vya dola kufanya kazi yake.

No comments

+255716829257