Habari mpya

Dogo Janja Afafanua video yake mpya ya Imani

 Dogo Janja ameamua kuweka wazi kuhusiana na kile ambacho ametaka kukifikisha kwa jamii kwenye ngoma yake mpya ya ‘Imani’ na hii ni baada ya kuonekana wengi kutoolewa kile ambacho kimefanywa na Dogo Janja kwenye video hiyo.
Dogo Janja ametumia ukurasa wake wa instagram kuelezea kile ambacho kinazungumzwa kwenye video ile ikiwa na kuonekana amevua nguo zake na kuvaa majani na kusema kuwa inafikia wakati mtu anapata shida nyingi zinazomsumbua kichwani kwake na kuamua kwenda sehemu ya mbali ili kuepuka yale anayomsumbua.
“Story ya VIDEO YA IMANI.. Nafikiri watu wanatakiwa waelewe story ilivyokua katika huu wimbo, “Mpaka kufikia yule mwanadamu anavua vitu vyake vya thamani anabakia na migomba tu isiyokua na thamani kwenye mwili wake.. Yule ni mtu ambae ana shida nyingi sana zinamsumbua kichwani kwake “Kazini” “Mapenzi” “Familia” “Marafiki” kwaiyo mwisho wa siku anaona bora atokomee sehemu yoyote mbali ambapo anakua haonani na mtu yoyote ambae anajuana nae”
“Lakini wakati anatembea kwa miguu Anachoka ule uchovu unamfanya anafikia hatua ya kulala sehemu yoyote ile, kwa bahati nzuri au mbaya anaamua tu bora “AJIUE,AFE” yaani asiwepo tena dunian😥 Anaamua kwenda kulala kwenye reli ili Treni ikipita imkanyage na asiwepo tena dunian😌… bahati nzuri MWENYEZI MUNGU bado anatamani huyu bwana aendelee kuishi hadi inafika Asubuhi hakuna hata Treni ambayo imepita kwaiyo anajikuta bado mzima, anashangaa.. kwaiyo anakasirika kwanini mimi bado mzima?”
“Siipendi hii DUNIA lakin naona bado inanifata fata Kwaiyo sasa anaamua kuvua vitu vyake vya thamani kuanzia NGUO ambazo zilikua na thamani ya juu “SUIT” akavua vitu vyote saa,cheni..boxer ili abaki mtupu kwa sababu anaamini akiwa mtupu DUNIA itakua inamshangaa, wakati dunia inamshangaa na yeye ndipo atapopata nafasi ya kuendelea na maisha mengine sehemu nyingine..kwaiyo anavua vitu vyake anava “MIGOMBA” ambayo haina thaman anaanza kutokomea, anatokomea sehemu ambayo anakutana na kijiji ambacho anakutana na watu ambao hawamjui ametokea wapi?”
“Wanamshangaa 😳 anatokomea porini anakutana na wanyama “NGAMIA” anatokomea tena porini anakutana na “MASHAMBA” kwaiyo mwisho wa siku inabaki ile Tafsiri yake “YEYE AMEICHOKA DUNIA,AMECHOKA VITU VILIVYOMO KWENYE DUNIA KAMA VITU VYA THAMANI” MARAFIKI,MAPENZI,FAMILIA… kwaiyo anaamua a-Disappear aondoke ambapo ye anazania anapoenda ndio kutakua na amani ya nafsi yake,lakini akiwa hana kitu chochote ambacho kitakua kinamsumbua duniani”
“So Ni IMANI ambayo yeye yuko nayo lakini mwisho wa siku tunasema TUNAPITIA, Na kila mtu ANAPITIA ups and down vitu vya kawaida sana ukiwa na imani Na Nai -dedicate kwenu leo wote”

No comments

+255716829257