Habari mpya

Wakili anaemtetea Mbowe, Viongozi 8 amejitoa, aeleza sababu

Wakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya amejito kuwatetea viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuamuru washtakiwa wasomewe Maelezo ya awali (Ph).
Mtobesya ameamua kujitoa katika kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali inayowakabili viongozi hao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Willbard Mashauri baada ya kuamuru wasomewe maelezo ya awali (Ph).
Amri hiyo ya mahakama imetokana na hoja ya wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kwamba kwa kuwa mahakama hiyo imetupilia mbali maombi ya utetezi kuhusu kuahirishwa kwa kesi hiyo wanaomba wawasomee washtakiwa (Ph).
Hata hivyo, hoja ya Nchimbi ilipingwa na wakili Mtobesya ambapo ameiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi August 27 kwa kuwa wateja wake hawakujiandaa kusomewa maelezo hayo.
Kutokana na mvutano huo, Hakimu Mashauri amesema anakubaliana na upande wa mashtaka kwamba Mbowe na wenzake wasomewe maelezo ya awali leo leo bila kuahirisha.
Kutokana na uamuzi huo, wakili Mtobesya alisimama na kueleza mahakama kuwa anajitoa kuwatetea Mbowe na wenzake akihisi hawatotendewa haki.
“Mheshimiwa Hakimu Mimi najitoa katika kesi hii kwani nikiendelea kuwawakilisha washtakiwa nahisi haki haitatendeka” ameeleza Mtobesya.
Kutokana na kujitoa huko, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi August 27,2018 ili washtakiwa wasomewe maelezo hayo.
Source: millardayo.com

No comments

+255716829257