Habari mpya

Viongozi wa serikali na wasanii wamlilia King Majuto


Alijizolea tuzo mbalimbali enzi za uhai wake
Image captionAlijizolea tuzo mbalimbali enzi za uhai wake

Msanii mkongwe na maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki Amri Athuman maarufu Mzee Majuto amefariki dunia wakati akipokea matibabu kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo Dar es Salaam Tanzania.
Muigizaji huyo veterani alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kufariki kwake.
Taarifa ya ikulu imesema King Majuto amefariki dunia majira ya saa 1:30 Jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Tayari watu maarufu ndani na nje ya Tanzania wametuma salamu za rambirambi kwa familia yake kupitia mitandao ya kijamii, miongoni mwao Rais wa Tanzania John Magufuli.
Rais Magufuli amesema King Majuto atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu alioutoa kupitia sanaa ya uigizaji na uchekeshaji, ambapo alishiriki kuelimisha jamii, kuendeleza na kukuza sanaa na kuunga mkono juhudi za chama na Serikali katika kuhimiza maendeleo.

Magufuli

"King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake," amesema Rais Magufuli.
Rais magufuli alimjulia hali msanii King Majuto alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam 31 Januari, 2018.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, ambaye pia ni mbunge wa Kigoma-Ujiji Zitto Kabwe amesema: "Nimepokea Taarifa ya msiba wa Mzee Majuto kwa masikitiko makubwa sana. Tumshukuru Mola kwa uwezo wake na kuwaombea wafiwa kwa mola awape subra."
Msanii maarufu wa bongo fleva Naseeb Abdul akijulikana zaidi kama Diamond Platnumz, ameandika kuwa Mzee Majuto ni mfalme ambae ataishi mioyoni mwa wengi daima.

DiamondHaki miliki ya pichaINSTAGRAM

Msanii Ali Kiba naye ameandika: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika Mzee Wetu Amri Bin Athuman (King Majuto) yuko katika dhima yako na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitina ya kaburi na dhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu. Amin."

Vanessa Mdee ni miongoni mwa walioandika ujumbe wa kumuomboleza kwenye mitandao ya kijamiiHaki miliki ya pichaINSTAGRAM
Image captionVanessa Mdee ni miongoni mwa walioandika ujumbe wa kumuomboleza kwenye mitandao ya kijamii

Akiwa kama mfalme wa tasnia ya maigizo ya uchekeshaji nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mzee Majuto aliweza kujizolea umaarufu mkubwa kupitia namna ambavyo alikua akiigiza na kuwa miongoni mwa watu wenye mvuto mkubwa miongoni mwa wasanii.

Aliweza kuvaa kila aina ya uhusika
Image captionAliweza kuvaa kila aina ya uhusika

Afya ya Mzee Majuto ilizorota zaidi kuanzia mwaka 2018 ambapo awali alipelekwa nchini India kwa matibabu baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli na wapenzi wa sanaa ya Mzee Majuto kumchangia ili kunusuru uhai wake kabla ya baadae kurejea nchini Tanzania.
Wiki chache zilizopita taarifa za uongo za kifo chake zilisambaa mitandaoni kabla ya familia yake kukanusha mara kwa mara.
Majuto aliyezaliwa mkoani Tanga Kaskazini mwa Tanzania mwaka 1948 alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka tisa.
Amecheza kwa mafanikio makubwa kwenye tamthiliya kama vile Mama Nitilie, Kondakta na nyinginezo nyingi zilizompa umaarufu mkubwa.

Akiwa na waziri wa sanaa Tanzania Harisson Mwakyembe ambaye alikua mstari wa mbele kupigania maslahi yake
Image captionAkiwa na waziri wa sanaa Tanzania Harisson Mwakyembe ambaye alikua mstari wa mbele kupigania maslahi yake

Kabla ya kifo chake tayari alikwisha wasamehe baadhi ya waandaaji na wasambazaji ambao inasemekana walikua wakimdhulumu mamilioni ya fedha baada ya waziri anayehusika na sanaa nchini Tanzania Harisson Mwakyembe kutishia kuwashitaki watu hao.
Atabaki kuwa nembo ya tasnia ya uigizaji wa vichekesho nchini Tanzania hata baada ya kifo chake.
UTARATIBU WA MAZISHI YA MZEE MAJUTO KATIKA VIDEO HAPA CHINI

No comments

+255716829257