Habari mpya

Uganda: Mahakama ya kijeshi yamfutia mashtaka Bob Wine

Mahakama ya Kijeshi nchini Uganda imemuondolea mashtaka Msanii na Mbunge Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi wine aliyekuwa ameshikiliwa kwa kipindi cha wiki moja.
Mbunge Bobi Wine alikuwa amefunguliwa mashtaka na Serilaki ya Uganda ya kumiliki na kupatikana na bunduki kinyume na sheria za nchi hiyo ambapo Mbunge huyo mwenye wafuasi wengi alikuwa tayari ameshawaajiri Mawakili kutoka Marekani kwa ajili ya kumuwakilisha kwenye kesi yake hiyo.
Hata hivyo baada ya Mahakama ya kijeshi kumuachi huru Bobi Wine alikamatwa tena na kufunguliwa Mashtaka ya uhaini katika Mahakama Kiraia (kawaida).
Inaelezwa kuwa kumekuwa na shinikizo kubwa la kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru ambapo nchini Kenya baadhi ya Wananchi wameandamana wakishinikiza Mbunge huyo aachiwe huru.

No comments

+255716829257