Habari mpya

Rais Magufuli alivyoshika Drip akimshusha Kingwangalla kwenye ndege

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala ambaye amesafirishwa kwa ndege kutoka Arusha alikopata ajali leo asubuhi, kuja DSM kwa matibabu zaidi.
Dkt. Kigwangalla amepata ajali leo majira ya saa 12:15 asubuhi katikati ya vijiji vya Mdolii na Minjingu Wilaya ya Babati Mkoani Manyara baada ya gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii Hamza Temba na wengine watano akiwemo Dkt. Kigwangalla kuumia.

No comments

+255716829257