Habari mpya

Yaliyojiri katika fainali za Ndondo Cup 2018

Michuano ya soka la mchangani kwa mwaka 2018 maarufu kama Sports Extra Ndondo Cup imehitimishwa siku ya Jumamosi ya August 5 2018 katika uwanja wa Bandari kwa kuzikutanisha timu za Manzese United dhidi ya Kivule United.
Mansese United wamefanikiwa kuwa mabingwa wapya wa michuano ya Ndondo Cup 2018 kwa kuifunga Kivule United kwa goli 1-0, michuano ya Ndondo Cup 2018 ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo RC wa DSM Paul Makonda, MD wa Clouds Media Joseph Kusaga, Mbunge wa Iramba Dr Mwigulu Nchemba na naibu waziri wa michezo Juliana Shonza ambaye alikuwa mgeni rasmi.

No comments

+255716829257