Habari mpya

Haya ndiyo aliyoyaongea waziri Lugola katika mkutano wake na waandishi wa habari..

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amezungumza na Waandishi wa Habari kuhusu matamko na maagizo mbalimbali aliyoyatoa tangu aapishwe kushika nafasi hiyo na Rais Magufuli.
Baadhi ya mambo aliyoyazungumza waziri huyo ni pamoja na haya yafuatyo;
“Nimemuagiza Mkurugenzi wa NIDA afike Ofisini kwangu Dodoma tarehe 25 akiwa na waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya Taifa kuja kunieleza kwa nini mtambo huo haujaletwa au waje na pesa walizopewa” – Waziri Lugola
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza IGP Sirro kumtafuta mmiliki wa Kampuni ya LUGUMI na kumfikisha ofisini kwake July 31 saa 2 asubuhi.
“Nimempa muda IGP Sirro na July 31 nitakutana na wadau wa usafirishaji kuzungumza nao wenye mabasi, wamiliki wa malori pamoja na madereva ili na wao wanipe mtazamo wao juu ya jambo hili la kutembea usiku” Waziri Lugola
“Nilipita kwenye kikosi cha farasi na mbwa ambao wanapewa mafunzo kama askari, kwenye vitabu vya makabidhiano nilikuta dosari ya idadi kubadilika siku moja na nyingine, nilitoa maagizo na IGP ameitisha uchunguzi, tuwape nafasi watupe majibu” Waziri Lugola
“Katika ziara yangu nilibaini mapungufu kutokana na makabidhiano ya Mbwa na Farasi. Ili kuhakikisha kikosi hiki kinaboreshwa, nimekubalina na IGP Sirro kufanya uchunguzi wa kina na wanipe maelekezo” – Waziri Lugola
“Kuhusu yule askari wa Kikosi cha Zimamoto aliyekuwa anazembea zembea basi tulimchukulia hatua kwa kumvua cheo kimoja kama salamu ili kusiwepo na kauzembe uzembe katika kazi” – Waziri Lugola
PropellerAds
Bado kumekuwa na baadhi ya askari wanaendelea kulichafua Jeshi la Polisi kwa kuwabambikizia wananchi makosa na kuwalazimisha kutoa rushwa, naomba niwaeleze watanzania, Askari akikikulazimisha umpe rushwa usitoe njoo utoe taarifa kwetu” – Waziri Lugola
“Ikitokea dereva yoyote amefikishwa Mahakamani bila ya kulazwa mahabusu huyo aliyekufikisha atawajibika yeye” – Waziri Lugola
“Nimekubaliana na IGP Simon Sirro kwamba waingie kwa undani sana kufanya uchunguzi wa kujua nini kimetokea kwenye kikosi cha Mbwa na farasi halafu wanipatie ufumbuzi. Hivyo naomba jambo hilo liachwe kwa kuwa lipo katika uchunguzi- Waziri Lugola
PropellerAds
Tazama video hapo chini waziri Lugola akiongea na waandishi wa habari

No comments

+255716829257