Habari mpya

JE UNAJUA KUWA KUFUNGA KUNAWEZA KUSADIA KUPUNGUZA UNENE KWA KIASI KIKUBWA??

Image result for KUNAWEZA KUSADIA KUPUNGUZA UNENE
Wengi wetu tunaposikia “kufunga” fikra inayokuja kichwani ni mwezi Ramadhani na dini ya Kiislamu. Ukweli hapa ukisema “unafunga” jambo la kwanza unaloulizwa ni kama wewe Mwislamu, kwamba huli nguruwe na kadhalika. Kinachosahaulika ni kwamba dini mbalimbali zina tabia na mtindo wa kufunga na kutokula.
Ila mfungo ninaouongelea si wa kidini.
Ni mfungo wa kusafisha, kupiga deki na kukarabati mwili.
Kawaida tunapokwenda haja kubwa si kila kitu hutoka. Mabaki tumboni husongana kule kwa miaka hatimaye huanza kutuletea vidonda tumboni, harufu mbaya ya mdomo, ushuzi wa kutisha, maradhi kama saratani ya utumbo mkubwa nk. Njia moja ya kupunguza adha hii ni kutokula kwa saa 36 kuendelea.
Kutokula kwa saa 36 kuendelea, mara moja mbili kwa mwezi husaidia sana mwili kupumzika. Wakati viungo vya ndani vikipumzika akiba iliyobakia bila kutumika hulazimika kutumika- na kile kilicho kibaya huondoka au kunyaushwa. Ndiyo maana baada ya kufunga kinyesi huwa na harufu mbaya sana. Faida kuu mbali ya usafi, ni baadhi ya virusi vinavyoushambulia mwili wetu kufa baada ya saa 21 ya mfungo. Hivyo, kama una mafua au aina fulani ya kikohozi si ajabu vikapotea. Hatujazungumzia kuvimbiwa kukitoa vile vile hapo!
Faida ya pili ni kuondokana na takataka zinazoingia kupitia puani (unapopumua) ngozi na uchafu wa mashine ulioko katika vyakula vya kisasa. Mboga na nyama tunazokula huwa siku hizi zimechafuliwa na mioshi ya magari, mashine, sigara, vumbi na viwanda. Kitaalamu vitu hivi vinaitwa “carcinogens” na moja ya sababu kuu za maradhi ya Saratani na wanawake kuzaa watoto wenye miili isiyo sawasawa(mathalan ubongo wa mtoto kua na upungufu). Hata unaposafisha vyakula hivi bado sehemu fulani huingia mwilini na si yote hutoka.
Unapofungua shurti uwe na matunda na sukari asilia ndani mathalan tende.
Unapofunga unasaidia kuchuja uchafu huo.
Tatu, faida ya kutokula kwa muda ni ngozi na nywele. Kwa kuwa sehemu kubwa ya vyakula tunavyokula imejazana mafuta na vitu vinavyobakia mwilini- unapofunga unasaidia usafi. Ngozi ya miili yetu ni kiungo kikubwa kuliko vyote sababu iko kila mahali na mishipa ya damu na nywele hutokezea chini yake. Kwa wanawake ambao hujali sana wajih wa ngozi zao- hili ni basi, jambo muafaka, si kidogo!
Nne, faida ya kufunga ni kupunguza mafuta na aghalabu unene.
Kwa hiyo wale wanaotaka kupunguza unene, wanaweza kufaidika kwa kufunga mara mbili tatu kwa mwezi.
Lakini lazima ufahamu namna ya kufunga.
Jambo muhimu si tu kujua uanze saa ngapi bali utakapofungua utaanzaje… kula.
Ni hatari sana kufunga saa 24 kisha ukaanza na milo mizito mizito (huku unabugia chakula) kwa kuwa ulikua na njaa. Unatakiwa uanze na maji, upumzike kidogo kisha matunda au tende na matunda, upumzike kidogo kisha ndo ule mlo mdogo au mboga na hatimaye baadaye kabisa chakula kizito cha wanga na protini. Kula milo mingi kwa wakati mmoja hakufai kabisa baada ya kufunga.
Mboga za majani zilizopigwa mvukwe bila kuivishwa sana- ni muhimu unapofungua. Hapa ni broccoli kwa matango. Wale wanaoweka chumvi ndani ya mboga mbichi wanakosea sana, maana ladha wanayoitafuta inawaharibia damu.
AINA YA UFUNGAJI
1. Unaweza kufunga saa 36- huku unakunywa maji. Baada ya kula mlo wako wa mchana mathalan, huli tena hadi kesho kutwa asubuhi. Kila unaposikia njaa au uchovu unakunywa maji moto taratibu. Hii inasaidia sana kuchuja figo. Unatakiwa unywe taratibu. Ukifungua unaanza na matunda laini ya “alkaline” ambayo ni rahisi kumenng’enywa – yaani mapapai, matikiti maji, maparachichi, matufaha, ndizi mbivu. Si vizuri kufungua kwa machungwa au mananasi maana yana uchachu.
2. Unaweza kufunga kwa kula tu matunda pia. Matunda chachu (acid) yaani machungwa, maembe, maembe, mananasi na kiwi yanaweza kusaidia kupunguza mafuta mwilini. Lakini usile mengi kama yale ya aina nyingine juu (namba 1).
3. Kufunga kwa kunywa mboga zilizotengenezwa kama uji. Bila chumvi au pilipili. Au kama ukiweka chumvi iwe kidogo sana. Ufungaji huu ni mzuri kwa kusaidia tumbo lililovimbiwa. Unaweza kuufanya kwa muda mrefu zaidi- saa 50 kuendelea.
4. Kufunga kwa kutokula chochote, saa 36 kuendelea.
Unapofunga namna hii, ni vizuri kufanya mazoezi ya kuvuta pumzi, mazoezi mepesi ya kujinyoosha au kujimwagia maji baridi mara kwa mara.
Kujimwagia maji ya (ndoo nzima toka utosini) kunaukumbusha mwili wakati mtu ulikuwa ndani ya tumbo la mamako. Enzi hizo za miezi tisa mwili ulitegemea bahari ya umaji maji ndani ya tumbo- hivyo unapojimwagia maji unaingiza maji kupitia ngozi.
Kwa wakazi wa nchi ziziso za joto kujimwagia maji ya baridi katika ndoo ni jambo muafaka linalojenga akili, mwili na ukakamavu. Maji hayo yanataiwa yawe ndoo nzima. Kitendo hiki kinatakiwa kifanywe kwa uangalifu sana. Kwanza kama una ugonjwa wa moyo usifanye maana maji baridi ya ndoo nzima yanaweza kuustua sana mwili. Pili kama hujazoea anzia tu kwa kujimwagia miguuni, au robo tu ya ndoo. Utamaduni huu umeenea sana nchi za Finland na Urusi ambapo wananchi kule huogelea katika maji baridi yenye barafu. Unasaidia sana kukomaza mwili na kujenga nguvu za Kinga Maradhi.
Ukilifanya wakati umefunga linakujenga sana na kusaidia mwili kupambana na magonjwa, kujenga nidhamu kiakili, kutokata tamaa na maisha, nk. Kifupi husaidia kiini cha uhai wako

No comments

+255716829257