YAJUE MADHARA YA UTUMIAJI WA MIRUNGI..
Na Ramadhani Gidion.
Vijana wengi wamejiingiza
katika utumiaji wa madawa ya kulevya aina ya mirungi bila kujua madhara yake kiafya.Mirungi
ni aina nyingine ya madawa ya kulevya. Mirungi huwa na majina mengine kama vile
miraa, mbaga, mogoka, veve, gomba, kashamba. Ingawa imekuwa ni tamaduni kwa
nchi za mashariki na saudia, Mirungi huathiri afya yako kwa kusababisha
madhara yafuatayo:
Magonjwa ya vidonda vya tumbo na mdomoni (peptic and oral ulcers);
Magonjwa ya vidonda vya tumbo na mdomoni (peptic and oral ulcers);
Ukosefu wa haja kubwa (constipation);
Utumiaji wa muda mrefu husababisha kuharibu utendaji kazi wa ini,
na pia kusababisha ubadilikaji rangi meno, kudhoofika, na fizi kuuma na harufu
ya mdomo;
Upungufu wa msukumo wa kufanya jimaa (sex drive). Na pia kuwahi
kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu;
Kupatwa na ugonjwa wa nyama au
vidonda sehemu za haja inayoota kwenye utupu wa nyuma;
Upungufu wa usingizi;
Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo (Addiction);
Walaji wengi huvuta na sigara, hata yule aliyekuwa havuti kabla ya
kuanza kula Mirungi, hujikuta akizama kwenye uvutaji, na madhara huwa maradufu;
Madhara ambayo bado kinamama
walaji Mirungi hawajagundua ni kwamba mtoto anayezaliwa na mama mlaji Mirungi
mara nyingi hukataa kunyonya titi la mama yake kwa sababu ladha ya maziwa
inabadilika kwa ajili ya utumiaji wa madawa (pesticides) unaotumiwa na wakulima
wa Mirungi kama inavyoeleza utafiti uliofanyika na Chuo Kikuu Cha Aden (Aden
University). Utafiti huo unazidi kueleza ya kwamba aina ya madawa yanayotumiwa
na wakulima ni zaidi ya 118 (na nyingi katika hizo ni katika zile zilizokatazwa
kisheria [illegal pesticides]) na ambazo zinasababisha asilimia 70 ya ugonjwa
wa saratani (cancer) huko Yemen.
Utafiti mwengine kule
Ethiopia unatueleza ya kuwa mtoto wa mama mwenye kula Mirungi kwa wingi huwa
hana uzito wa kawaida wakati wa kuzaliwa.
Ukosefu wa hamu ya kula chakula
na mengi mengine.
CHANZO: AFYA KWANZA.
No comments
+255716829257