SABABU ZISIZOFAA KUMFANYA MTU KUOA AU KUOLEWA.
Ndoa inasemekana ni
baraka pale wachumba wanapokuwa wamependana kwa dhati,
na kwa hiari yao
wanaona ni muda muafaka kuwa kitu kimoja kama mke na mume.
Lakini kwa upande
mwingine ndoa inakuwa ni balaa na kupoteza maana pale wachumba wanapoamua
kuingia katika ndoa bila sababu za msingi wala vigezo vya maana kati yao.
Yaani kila mmoja
anaingia na sababu na mkakati wake tofauti na alionao mwenzake.
Hebu tupeane sababu
mbovu kabisa ambazo kama utazitumia kama kigezo cha kufunga ndoa na mtu basi
andika umeumia:
Na Ramadhani
Gidion#mswahili.
1.UMRI WANGU UNAZIDI KUWA MKUBWA:
Hasa wanawake eneo hili ndio linawagusa sana kwani mara nyingi
wanajitahidi kukimbizana na muda,
na wanaweka mkakati kabisa kwamba nikifikisha umri fulani lazima
niwe ndani ya ndoa.
Ya inawezekana unatumia kigezo cha kuwahi kabla hujapoteza
muonekano lakini nakuambia wazi kabisa kama unaingia katika ndoa kwasababu hii,
andika maumivu siku zijazo.
Si kwamba usipoolewa basi wewe si mwanamke na kwamba ni mbaya,
hapana
ndoa ni taasisi ambayo si kila mtu amepewa uwezo wa kuwa
mwanachama kwahiyo ikija nafasi ya wewe kuwa mwanachama ingia bila matatizo
lakini si kujidai unakimbizana na muda.
2.MALI AU UTAJIRI WA MWANAUME/MWANAMKE:
Kipindi cha nyuma jamii ilishazoea kwamba mwanamke kuolewa na mtu
hata asiyempenda kwa kigezo cha mali za huyo jamaa ni kitu cha kawaida,
lakini bwana siku hizi hadi wanaume nao kigezo hiki wanakitumia
ili kutoka kimaisha.
Na ombea huyo unayemdanganya asijue kabla hujafaidika kwani akijua
atakuwahi na utakuwa umekosa ulichotaka.
Na wengi wao wanakumbana na mateso makubwa sana wanapoingia katika
ndoa na mtu kwasababu ya mali za huyo mwenzake.
3.NILINGANE NA RAFIKI ZANGU:
Sababu hii huwa ni asili kwani mara nyingi binadamu tumekuwa na
hulka ya kujilinganisha na wenzetu.
Sasa unapotaka kuingia katika ndoa kwa haraka kwa kuwa tu rafiki
yako ameolewa juzi unajitia matatizoni mwenyewe.
Wengi sana wanapata mshawasha pale wanapohudhuria sherehe za
harusi za ndugu na marafiki na shamra shamra za ukumbini kwa usiku huo
zinawadanganya na kudhani hiyo ndio ndoa na huku kichwani akijenga wazo la yeye
pia kutafuta mtu kwa haraka ili afanye kama mwenzake.
4.NJIA YA KUIMARISHA UHUSIANO:
Hapa wengi wanatumia sababu hii kulazimisha ndoa pale wanapoona
mahusiano yao katika kipindi hicho sio mazuri sana kwahiyo wanaona njia pekee
ni kuingia katika ndoa haraka ili kubadilisha mazingira pengine mambo
yatanyooka na kumtuliza mwenzake.
Kama utatumia sababu hii kujifunga kitanzi basi umeingia chaka
kwani sio sababu ya msingi kukufanya ulazimishe ndoa.
Kama katika kipindi hiki cha uchumba mnatofautiana si kwamba ndoa
ndio itawafanya muwe na mtazamo mmoja kihisia na maamuzi.
5.NATAKA TUWE KARIBU ZAIDI:
Wachumba ambao wanaishi mbali mbali wanadhani kuingia katika ndoa
haraka ni njia ya kumaliza umbali baina yao.
Na maamuzi haya mtu anaweza kuyafanya hata kwa kuhama mji na
kuhamia alipo mwenzake na kuanza kulazimisha ndoa hata kama mwenzake
hajaonyesha utayari.
"Oh! nimechoka kuwasiliana naye kwenye simu kila siku bora
nimfuate huko huko aliko na nimlazimishe anioe"
Kweli yawezekana unaumia lakini lazima uzingatie umbali wenu
unaletwa na nini,
na ukishagundua shirikiana na huyo mwenzako namna ya kutatua
ndio utajua kama na yeye yuko tayari na huo mpango wako au la
na sio kumvamia alipo na kulazimisha mambo.
6.NIONDOKE KATIKA NYUMBA YA FAMILIA:
Sababu nyingine mbovu ni hii hapa na jua wazi si sababu nzuri
kuitumia ili kuingia katika maisha ya ndoa.
Kuwa na subira ni kitu kizuri,
kama uliweza kulelewa hapo nyumbani kwenu kwa miaka mingi ndoa
isiwe kigezo cha kukuondoa.
Kweli kiumri umekua na unatamani uwe kwako ambako utakuwa una
maamuzi ya leo unafanya nini au unapika nini.
Na hapa inatokea mara nyingi pale msichana anapotembelea sehemu
anayoishi mvulana na kukuta jamaa kiasi fulani kajipanga na anatamani ahamie
hapo haraka kwa kumlazimisha ndoa,
kwani anaona kashapata njia ya mkato.
7.KISASI KWA ULIYEACHANA NAYE:
Hapa napo wananasa wengi sana,
yaani utakuta mtu anaachana na mchumba mwezi mmoja nyuma na
kwakuwa alimpenda na anataka kumlipizia kisasi basi analazimisha kuingia katika
ndoa na mtu mwengine ambaye hajakaa naye hata mwaka kumfahamu.
Hii ni moja ya sababu ya kijinga zaidi kutumia ili kufunga ndoa
kwa haraka,
kwani hautakuwa unamkomoa huyo unayetaka umkomoe bali utakuwa
unajiingiza katika matatizo wewe mwenyewe.
Kutoka:LISHA UBONGO.
No comments
+255716829257