NI MARUFUKU KUKATA TAMAA, ZINGATIA HAYA..
Na
Ramadhani Gidion#mswahili.
Katika maisha kuna wakati ambapo mambo
huwa magumu sana. Ni katika nyakati hizi ambapo watu wengi hukata tamaa na
kuacha kile ambacho walikuwa wanafanya. Kwa kukata tamaa unashindwa kufikia
mafanikio na pia unaona maisha yako kama hayana maana.
Leo JIONGEZE na sababu hizi
tano kwa nini ni marufuku wewe kukata tamaa.
Bado hujafa. Kama bado unaishi hii ina maana kwamba kila kitu
kinawezekana. Hata iwe umeshindwa au kupoteza kiasi gani, jipange tena na
utafikia mafanikio.
Kuna watu wengine walishafanya. Katika jambo lolote ambalo linakushinda kufanya, kuna
watu wengine walipitia changamoto kama zako ila waliweza kufikia mafanikio. Na
kwa bahati nzuri sana watu hawa wameandika yote hayo kwenye vitabu, vitafute na
uvisome.
Kuna watu wana hali mbaya kuliko wewe. Wakati wewe unalalamika huna viatu kuna mwenzako hana
miguu kabisa. Hivyo kukata tamaa na wakati kuna watu wana matatizo makubwa
kuliko wewe na bado wanaishi utakuwa hujitendei haki. Katika maisha kuna wakati
ambapo mambo huwa magumu sana. Ni katika nyakati hizi ambapo watu wengi hukata
tamaa na kuacha kile ambacho walikuwa wanafanya. Kwa kukata tamaa unashindwa
kufikia mafanikio na pia unaona maisha yako kama hayana maana.
Utawahamasisha wengine. Kama
ukiweza kufikia mafanikio licha ya changamoto unazokutana nazo utawahamasisha
wengine nao kuweza kufikia mafanikio. Kama utakata tamaa na kuacha utawakatisha
na wengine tamaa na kuwafanya wasijaribu kabisa.
No comments
+255716829257