JINSI YA KUTENGENEZA JIUSI YA NYANYA NA FAIDA ZAKE.
MAHITAJI.
Nyanya kubwa 8
1.
Jira
(cumin seeds) vijiko vya chai viwili
2.
Pilipili
manga nyeusi ya unga (black pepper powder) robo kijiko cha chai
=>
Safisha nyanya vizuri, nyanya zilizoiva vizuri lakini siyo zilizoiva sana.
Iondoe sehemu ya juu ya nyanya (kikonyo), kata vipande
vidogo vidogo na utumbukize kwenye blenda, ongeza mbegu za jira na maji kidogo na kisha uzisage kwa
pamoja.
Mwishoni
ongeza kiasi kidogo cha pilipili manga nyeusi ya unga. Koroga vizuri, chuja na
chujio juisi yako, mimina kwenye glasi na Unywe.
Faida 7 za Juisi ya Nyanya
1 . Husaidia kuulinda mwili dhidi ya kolesteroli
2
. Juisi ya nyanya ina kiasi kingi cha vyanzo vya vitamini A na C
3 . Faida nyingine kubwa ya juisi ya nyanya ni uwezo wake
katika kukusaidiakupunguza uzito uliozidi mwilini.
4
. Kama kuna juisi nzuri kwa mwili basi ni juisi ya nyanya, na ndiyo maana
nyanya ni kiungo kwa karibu kila mboga jikoni.
5
. Juisi ya nyanya pia ina kiasi kingi cha Vitamini B6
6
. Juisi ya nyanya huondoa sumu kwa urahisi zaidi mwilini sababu ina kiasi cha
kutosha cha klorine na sulfur
7 . Rangi nyekundu katika nyanya ni matokeo ya kimiminika
mafuta kiitwacho ‘lycopene’ ambacho kazi yake kuu ni kuondoa sumu
mwilini.
No comments
+255716829257