EPUKANA NA VISUNZUA{ SKIN TAGS/WARTS }..
Visunzua ni vinyama vidogovidogo
vinavyoota juu ya ngozi, hili ni tatizo la watu wengi kwa sasa, wanawake na
wanaume huwatokea. Inasemekana visunzua hutokana na tatizo la homoni mwilini,
unene uliopitiliza, kisukari na mabadiliko wakati wa mimba.Watu wengi
wanahangaika kutafuta tiba ya visunzua bila mafanikio. Nitakueleza vitu ambavyo
unaweza kuandaa mwenyewe nyumbani kukabiliana na tatizo hili na likaisha ndani
ya muda mfupi. Vitu vingine ukivisoma hapa utastaajabu maana huwezi
kufikiria vinaweza kuwa tiba
1.KITUNGUU MAJI NA APPLE CIDER
1.KITUNGUU MAJI NA APPLE CIDER
Kata vitunguu katika slice weka
kwenye bakuli ,changanya na apple cider kisha viache vilowane usiku
kucha,asubuhi chukua vitunguu bandika kwenye visunzua kisha funga vizuri na
plasta visitoke acha kwa masaa 4 hadi matano.Fanya hivi kila siku kwa muda wa
wiki moja utajipenda
2.KITUNGUU SAUMU,BAKING SODA NA LIMAO
2.KITUNGUU SAUMU,BAKING SODA NA LIMAO
Menya kitunguu saumu ,kisage kiwe
laini changanya na baking soda kijiko kimoja kisha changanya na
limao.Paka mchanganyiko kwenye sunzua ukiweza funga na plasta,kaa kwa
masaa mawili hadi matatu osha. Paka mara 3 kwa siku. Ni vizuri usiku ukilala
nayo. Baada ya muda mfupi utapata matokeo mazuri
3.ASPIRIN
3.ASPIRIN
Ni ile aspirin, dawa ambayo humezwa
Kwa kutuliza maumivu, hapa huimezi.unaiponda upate unga kisha changanya
na matone ya maji ilainike.paka kwenye sunzua Mara tatu hadi nne kwa siku.
Baada ya wiki utajifurahia
4.RANGI YA KUCHA
4.RANGI YA KUCHA
Sio tu urembo was kucha ,hapa rangi
inafanya kazi nyingine.paka rangi kwenye sunzua mara tatu hadi nne kwa
siku.usiku unashauriwa kulala nayo na ubandue asubuhi kwa wiki.
5.GANDA LA NDIZI
Bandika sehemu ya ndani ya ganda la ndizi na
usugue kwenye sunzua Mara nyingi uwezavyo kwa siku .ili upate matokeo mazuri
bandika plasta na uiache kwa muda mrefu.5.GANDA LA NDIZI
No comments
+255716829257