CHANZO NA TIBA ASILIA YA TATIZO LA KIPARA.
Katika miaka ya hivi karibuni,
suala la upara ( baldness ) linatajwa
kuwasumbua vijana wengi wa kiume. Miaka
ya tisini kurudi chini ilikuwa ni
aghalabu sana kumuona kijana wa miaka
25 akiwa na upara, na mara nyingi
suala la upara lilikuwa likihusishwa na
uzee,lakini leo hii hali ni tofauti
sana, kwani kuna idadi kubwa sana ya
vijana wa kiume wenye umri wa kuanzia
miaka 25 hadi 45 wana okabiliwa na tatizo
la upara. Pamoja na kwamba, kutokuwa na
nywele hakuwezi kukamfanya mwanadamu akashindwa
kuishi, lakini katika dunia ya sasa ya
mitindo na utandawazi kuwa na upara
ni jambo linalo wapa shida sana
wahusika.
KIPARA
HUSABABISHWA NA NINI ?
Yapo mambo mengi sana ambayo
ndio chanzo cha watu kuwa na upara .
Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo :
i. Kurithi
kutoka kwa wazazi ( Sababu za
kijenetiki )
ii. Lishe
mbovu
iii. Ukosefu
wa Vitamin B6
iv. Kuwa
na stress, mfadhaiko na mshuko wa
moyo kwa muda mrefu
NINI TIBA
YA TATIZO LA KIPARA??
Kama unasumbuliwa na tatizo la
kipara, jaribu tiba hii, inawaweza kuwasaidia
kama ilivyo wasaidia watu wengine.
i. Indian
gooseberry oil: Mafuta haya hutayarishwa
kwa kuyachemsha kwenye mafuta ya nazi.
Yanasaidia sana katika kuzifanya nywele
zikue vizuri. Vilevile mafuta haya yanaweza
kuchanganywa na juisi ya ndimu na kasha
kuyatumia kama shampoo, ukifanya hivi
itasaidia katika kuchochea ukuaji wa nywele
na kuzuia kukatika kwa nywele.
Margosa: Majani ya Margosa yana faida kubwa sana kwa mtu anaye taka kujitibu tatizo la upara. Mafuta haya yanaua chawa na vijidudu wengineo na kuzifanya nywele kuwa ndefu.
Tui la Nazi : Fanya masaji ya kichwani kwa kutumia tui la nazi. ( Masaji hii ifanyike katika sehemu yenye kipara )
Kitunguu Maji : Kata kitunguu maji, kichovye kwenye asali na ukitumie kujisugua kwenye sehemu iliyo athirika. Fanya hivyo mara tatu kwa siku.

SOURCE: NEEMA
HERBALIST & NUTRITION
No comments
+255716829257