Habari mpya

WALIOFANYA VIZURI KWENYE LIGI KUU TANZANIA BARA WAMETUNUKIWA ZAWADI HIZI HAPA..



Julai 16 waDhamini wa ligi kuu Tanzania Bara, Vodacom walitoa tuzo kwa wachezaji na makocha waliofanya vizuri kwenye ligi hiyo msimu wa 2015/16.
Spain
Zawadi zilizotolewa ni pamoja na zawadi ya bingwa wa ligi kuu, Yanga (sh.81,300,000), makamu bingwa, Azam FC (40,000,000), mshindi wa tata, Simba (sh.29,000,000), mshindi wa nne, Tanzania Prisons (sh.23,200,000), timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.
Mchezaji wa Yanga, Juma Abdul amefanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora na kukabidhiwa kiasi cha shilingi 9,000,000 na kuwashinda wachezaji aliokuwa wanawania tuzo hiyo akiwemo Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar) na Mohamed Hussein (Simba).
Tuzo ya mchezaji bora chipukizi imekwenda kwa Mohamed Hussein (Simba) aliyekabidhiwa kiasi cha shilingi 4,000,000 huku akiwashinda wachezaji wengine waliokuwa wakiwania tuzo hiyo akiwemo Farid Mussa (Azam), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).
Naye mchezaji wa Yanga, Thabani Kamusoko amekabidhiwa kiasi cha shilingi 5,740,000 baada ya kuibuka kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kigeni kwa kuwashinda wachezaji wengine wa kigeni kama Donald Ngoma (Yanga) na Vincent Agban (Simba).
Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm alitangazwa kama kocha bora kwenye tuzo hizo nsa kufanikiwa kupewa zawadi ya kiasi cha shilingi 8,000,000 na kuwashinda makocha wengine aliokuwa anashindana nao akiwemo Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons).
Hamis Tambwe wa Yanga alifanikiwa kupata tuzo ya mfungaji bora kwenye msimu ulioisha, huku Ibrahim Ajib wa Simba akifanikiwa kushinda tuzo ya goli bora. Mwamuzi Ngole Mwangole akifanikiwa kuibuka na tuzo ya kuwa mwamuzi bora kwa kuwashinda waamuzi wengine kama Anthony Kayombo na Rajab Mrope.
CHANZO: Bongo5

No comments

+255716829257