Uganda na Tanzania wajadili bomba la mafuta

Uganda na Tanzania zimeanza upya
mazungumzo utekelezaji wa makubaliano baina ya viongozi wa mataifa
hayo mawili kupitisha mradi wa bomba la mafuta kupitia Hoima Tanga
badala ya Hoima - Lamu Kenya.
Ujumbe wa Uganda unaongozwa na waziri wa kawi Irene Muloni huku Tanzania wakiongozwa na Prof Sospeter Muhongo.
Wengine wanaohudhuria mazungumzo hayo huko Hoima ni wawakilishi wa kampuni ya kuchimba mafuta yenye asili yake nchini Uingereza Tullow, mjumbe wa kampuni ya kuuza mafuta ya Total yenye asili yake nchini Ufaransa na kisha
kampuni ya kichina ya CNOOC inayotekeleza mradi wenyewe wa kuchimba na kuweka bomba la mafuta Kuanzia Hoima hadi bandari ya Tanga.

Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga.
Mada kuu ya mazungumzo hayo huko Hoima ni utekelezaji wa miradi kwa kuzungumzia hali halisia.
Kwa mfano maswala ya ardhi itakayotumika kwa mradi huo itamilikiwa na nani na itatwaliwa vipi kutoka kwa uma, pia kuna swala la ukubwa wa ardhi yenyewe, wanadani wanasema kuwa mradi huo ulikuwa umependekezwa utekelezwe kwenye ardhi ya takriban mita 20 ,sasa hilo linaonekana kupata upinzani na hivyo kunahoja mbadala ukubwa huo upunguzwe katika mradi huo utakaotekelezwa kwa umbali wa kilomita 1403.

Kenya iliamua kujenga bomba la mafuta kutoka Turkana hadi Lamu
Aidha swala la ujenzi wa mtambo wa kusafishia mafuta wenye thamani ya dola bilioni 2.5 uliopata pigo baada ya Serikali ya Uganda kukatiza mazungumzo na kampuni moja ya Urusi pia utajadiliwa.
Uganda imeanza mazungumzo mbadala na kampuni moja ya ujenzi kutoka Korea Kusini.
Uganda ilikuwa imependekeza kujenga bomba la mafuta safi mkabala na bomba la mafuta la Hoima -Tanga.
Mkurugenzi wa usafirishaji wa mafuta nchini Uganda Robert Kasande akizungumza na wanahabari alisema kuwa tayari wajumbe wamekubaliana mambo mengi kati ya maswala makuu yaliyohitaji kujadiliwa.
Uganda yavunja mkataba na kampuni ya Urusi
Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania
CHANZO: BBC
No comments
+255716829257