Habari mpya

Serikali imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake badala yake kuelekeza gharama hizo kwa wateja wao..

 
Mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' imetoa ufafanuzi kuhusu kodi ya ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha kuwa marekebisho ya sheria ya mwaka 2014 yaliyopitishwa na bunge yanayolenga kutoza kodi la ongezeko la thamani kwa kiwango cha 18% kwenye ada ambazo benki inatoza wateja wake kwenye huduma mbalimbali zitolewazo na benki au taasisi za fedha.

Katika taarifa maalumu kwa vyombo vya habari TRA wamesema taasisi za fedha wanapoongeza makato ya miamala ya fedha wanakosea kwa kupandishia wananchi kwa kuwa sheria hiyo inahusu fedha ambayo mwanachi alikuwa anakatwa na taasisi hizo ambayo hapo mwanzoni zilikuwa azilipiwi kodi kwa hiyo hizo ndizo zitakazokatwa 18%


Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa asilimia 18 ya VAT mpya iliyopitishwa kwenye miamala ya benki inahusisha gharama zilizokuwa zikitozwa na benki hizo kwa wateja wao lakini serikali ilikuwa haipati chochote. 

Kidata amesema kuwa Benki Kuu imeelekezwa kudhibiti benki hizo kwa kufanya ujanja wa kuongeza makato kwenye miamala ya wateja wao wakati wakijua fika kuwa hilo si lengo la kodi hiyo mpya.

Ameelekeza kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye miamala hiyo kinatakiwa kubaki kama mwanzo lakini serikali itakata kodi yake ya asilimia 18 na kodi nyingine zilizopo kwa mujibu wa sheria.


Aidha Kadata ametoa  Mfano"kama umetoa fedha ukakatwa 1000 na taasisi ya fedha ilikuwa haikatwi kodi lakini kwa sheria hiyo ada hiyo ndio itakatwa 18% na sio mwananchi kuongezewa makato kama ilivyofanyika kwa baadhi ya taasisi za fedha",Kadata.

[​IMG]
Tazama video hapa chini.

No comments

+255716829257