Serikali ya Tanzania imeyafutia usajili magazeti 473 leo..
Serikali imefuta usajili wa Magazeti 473
kupitia tangazo lililochapishwa katika gazeti la serikali lenye namba
195 ambapo sababu za kufutwa usajili huo ni kutochapishwa kwa muda wa
miaka mitatu mfululizo.
Magazeti
hayo hayataruhusiwa kuchapishwa au kusambazwa kwa njia ya nakala ngumu
au kielektroniki na ikiwa mmiliki wa gazeti lililofutiwa usajili
angependa kuendelea na biashara milango iko wazi kwa ajili ya
kuwasilisha maombi mapya ya usajili kwa kufuata taratibu zilizopo.
Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya msajili wa magazeti, nchi ya Tanzania inayo magazeti na majarida 881 yaliyosajiliwa kisheria.
chanzo: millardayo.com
No comments
+255716829257