PERUZI HABARI KUU ZA ULIMWENGU LEO JULY 20, 2016..
1. Trump asema anajivunia kuwa mgombea Marekani
Donald Trump ameuambia mkutano wa kitaifa wa chama cha Rebuplican mjini Cleveland kwamba anajivunia kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi wa urais mwezi Novemba.
Akizungumza katika ujumbe kwenye kanda ya video, Trump amesema atashinda kura hiyo na ataleta mabadiliko halisi kwa Washington.
Spika wa bunge la wawkilishi, Paul Ryan, ameomba wajumbe kwenye kikao hicho kumuunga Trump mkono akieleza kuwa kutakuwa na uhakika wa ushindi iwapo tu wanachama wote wa Republican watashirikiana.
2. Watu 50,000 waadhibiwa Uturuki
Watu wapatao 50,000 wamefutwa au kusimamaishwa kazi na serikali ya Uturuki kufuatia jaribio lililotibuka la mapinduzi wiki iliyopita.
Wanajeshi, Polisi na maafisa wengine wamelengwa kwa kuonekana kutomtii rais na walimu, wahadhiri katika vyuo vikuu na watu wanaofanya katika vyombo vya habari pia wamelengwa.
3. Mwezi Juni wavunja rekodi ya joto
Wanasayansi wanasema mwezi uliopita ulikuwa na joto zaidi ya miezi mingine katika siku za nyuma huku kiwango cha kadiri cha joto katika miezi sita ya kwanza mwaka huu duniani kikiwa nyuzi joto moja na nusu zaidi ya viwango vya enzi za kabla ya kuenea kwa viwanda viwanda.
Makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yalioafikiwa mwaka jana yalinuiwa kusitisha ongezeko la joto kwa kiwango kama hicho.
4. Ufaransa yatarajia mashambulio zaidi
Waziri mkuu wa Ufaransa amesema taifa lake ni lazima litatarajie mashambulio zaidi ya kigaidi na vifo zaidi licha ya hatua za tahadhari zinazochukuliwa na serikali.
Akizungumza katika mjadala ampapo bunge la kitaifa limeidhinisha kuongezwa hali ya tahadhari nchini kwa miezi sita, Manuel Valls amesema Ufaransa inabidi ijifunze kuishi na tishio kama lile la shambulio la Nice.
5. Maafisa Florida wabuni njia ya kuabili Zika
Maafisa wa afya katika jimbo la Florida Marekani wanaunda vyenzo vya kujikinga dhidi ya virusi vya Zika na kuvisambaza katika eneno la Miami-Dade, kufuatia kutokea kwa uwezekano wa kisa cha maambukizi katika eneo hilo.
Maafisa wanasema wanachunguza kisa ambacho hakionekani kutokana na mtu kusafiri katika eneo jingine.
6. Wanaocheza Pokemon Go Bosnia waonywa
Raia wanaocheza mchezo mpya wa simu waPokemon Go nchini Bosnia wameonywa dhidi ya kufika katika maeneo yalio na mabomu ya ardhini yalioachwa baada ya mzozo wa kivita katika miaka ya 90. Shirika la kutoa misaada la Posavina bez mina limewaomba watu kuheshimu maeneo yaliowekwa alama ya kutopita, na kwamba wasiende katika maeneo wasiyoyafahamu vyema.
No comments
+255716829257