Habari mpya

PERUZI HABARI KUU ZA ULIMWENGU LEO JULY 19, 2016..

1. Melania asema mumewe Trump atafaa Marekani

 
Mkewe Donald Trump, Melania, ameuambia mkutano wa kitaifa wa chama cha Republican kwamba mumewe ni mshindi ambaye hawezi kuiangusha Marekani.
Mwanamitindo huyo wa zamani aliyezaliwa Slovenia, alikuwa mzungumzaji mkuu katika siku ya kwanza ya kikao hicho mjini Cleveland.
Awali kulikuwa na ghasia wakati wajumbe walipopiga kelele na kuzomea kukataliwa ruhusa kudhihirisha upinzani wao kwa Trump kuwa mgombea.

2. Mhamiaji ashambulia abiria kwenye treni Ujerumani

 
Maafisa nchini Ujerumani wanasema mhamiaji mwenye umri wa miaka 17 kutoka Afghanistan
amewashambulia watu wanne katika treni karibu na mji uliopo kusini Würzburg.
Mshambuliaji huyo ambaye baadaye alipigwa risasi na kuuawa na polisi alikuwa na shoka na kisu.
Watu watatu wamo katika hali mahututi, huku wengine 14 wanatibiwa kwa mshtuko waliopata.

3. Erdogan asema hawaadhibu wapinzani wake


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema fununu kwamba anawaadhibu wapinzani wake wa kisiasa kufiatia jaribio la mapinduzi wiki iliyopita, ni tuhuma zinazomchafulia jina.
Kiasi ya maafisa 18,000 wa polisi wa jeshi na majaji wamesimamishwa kazi au kukamatwa tangu kutibuliwa jaribio hilo la mapinduzi.

4. Waziri wa Ufilipino akataa pendekezo la Uchina

 
Waziri wa mambo ya nje wa Ufilipino amesema amekataa pendekezo kutoka waziri mwenzake wa China kufanya mazunguzmo ya pande mbili kuhusu mzozo wa umiliki bahari ya China kusini kwa sababu China imesisitiza kuwa uamuzi uliopitishwa wiki iliyopita wa jopo la kimataifa haupaswi kuwa sehemu ya majadiliano hayo.

5. Korea Kaskazini yarusha makombora

 
Korea kusini na Marekani zinasema Korea Kaskazini imerusha makombora matatu ya majaribio kwenye bahari pwani yake ya mashariki.
Ni zaidi ya wiki moja tu tangu Pyongyang kutishia kuchukua hatua dhidi ya mpango wa Marekani kutuma makombora kusini.

6. Aliyeua askofu Guatemala afariki

Maafisa Guatemala wanasema afisa wa jeshi aliyehukumiwa kwa mauaji ya askofu maarufu wa Kikatoliki amefariki katika ghasia zilizozuka gerezani.
Byron Lima alikuwa anatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani kwa maauji hayo aliyoyatekeleza mnamo mwaka1998 ya Askofu Juan Jose Gerardi, aliyekuwa mpinzani wa utawala uliokuwepo wa kijeshi.
Inaarifiwa kuwa Lima alikuwa mmojawapo ya wafungwa wenye nguvu na ushawishi katika magereza ya Guatemala.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257