PERUZI HABARI KUU ZA ULIMWENGU LEO JULY 12, 2016..
1. May aahidi Uingereza itajitoa vyema EU
Theresa May, Mwanamke atakayekuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza Jumatano, ameahidi kufanikisha hatua ya taifa hilo kujitoa katika muungano wa Ulaya, licha ya kuunga mkono kusalia katika EU kwenye kura ya maoni mwezi uliopita.
Bi May amesisitiza kuwa kuna haja ya kujadiliana mpango ulio bora, na ameahidi uongozi madhubuti kuliongoza taifa hilo katika wakati mgumu kiuchumi na kisiasa.
2. Kiir na Machar watangaza kusitisha vita
Pande zote katika mzozo wa Sudan kusini zimetangaza kusitisha mapigano.
Makamu wa rais, Riek Machar, ameiambia BBC kwamba ghasia zilizozuka ni kutokana na anachokitaja kuwa mpango ualiotekelezwa na watu waiotaka amani.
3. Mkuu wa polisi Dallas asema silaha ni tatizo
Mkuu wa polisi katika mji wa Dallas Marekani ameeleza kuwa sheria za jimbo la Texas zinazoruhusu raia kubeba silaha wazi zinasababisha matatizo katika kuidhinisha sheria.
David Brown alikuwa akizungumza kufuatia kupigwa risasi na kuuawa kwa maafisa watano wa polisi wiki iliyopita na aliyekuwa afisa wa jeshi.
4. Venezuela kutwaa kiwanda cha Marekani
Serikali ya Venezuela imesema itadhibiti kiwanda kinachomilikiwana kampuni ya Marekani, Kimberly-Clark, baada ya kampuni hiyo kutangaza kuwa haiwezi tena kuendesha biashara nchini humo.
Waziri wa Leba Venezuela amesema hatua ya kukifunga kiwanda hicho ni kinyume na sheria na inakiuka haki za wafanyakazi wapatao 1000.
Kimberly-Clark imesema imekuwa vigumu kufanya kazi Venezuela kwasababu ya udhibiti mkali wa sarafu, ukosefu wa bidhaa kuu na kuongezeka kwa kiwango kikubwa kwa bei za bidhaa.
5. Israel yaidhinisha sheria kudhibiti mashirika
Bunge la Israeli limepitisha sheria inayokumbwana mzozo inayohitaji mashirika yasio ya kiserikali kutoa taarifa kuhusu ufadhili wa nje iwapo zaidi ya nusu ya ufadhili wao unatoka serikali au taasisi za chi za nje.
Wanaopinga sheria hiyo wanasema imenuiwa kuzuia ufadhili unaofikishwa kusaidia Palestina.
6. Vifaa vilivyotumiwa na tumbili Brazil
Wachimbaji ardhi wamegundua ushahidi wa vifaa vya jadi vya ujenzi vilivyotengenezwa kwa mawe vilivyotumiwa na tumbili huko Brazil.
Kulingana na ushahidi wa kutumiwa vifaa kwa viumeba tofauti kando na binaadamu, wakiwemo tumbilihadi kunguru.
Watafiti waligundua vifaa hivyo ambavyo vinaaminika kutumika na nyani kuvunja karanga, na vinavyoaminika kutumiwa takriban miaka 700 iliyopita.
CHANZO: BBC
No comments
+255716829257