NETANYAHU KUHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI ETHIOPIA..
Waziri Mkuuwa Israel benjamin
Netanyahu anakamilisha ziara yake barani Afrika Alhamisi nchini Ethiopia
ambapo anatarajiwa kukutana na viongozi wa serikali na kutia saini
mikataba kadhaa ya maendeleo. Tangu kuwasili kwake barani Afrika Julai
4, Netanyahu amezuru Uganda, Kenya na Rwanda katika kile alichokitaja
kama histori kubwa kwa Israel kurejea barani Afrika. Amekuwa Waziri mkuu
wa kwanza wa Israel kuzuru Afrika katika kipindi cha miaka thelathini.
Ethiopia
ilikuwa mojawapo ya nchi za kwanza barani Afrika kuanzisha uhusiano wa
kidiplomasia na Israel katika miaka ya sitini. Lakini uhusiano huo
umeyumba yumba mara kadhaa baada ya Ethiopia kuukatiza mara kadhaa
katika historia yake.Hii ilidhihirishwa zaidi wakati wa vita vya Waarabu na Israel mwaka 1973 wakati Ethiopia iliposimama pamoja na mataifa mengine ishirini ya Afrika; kukatiza uhusiano kidiplomasia na Israel. Hata hivyo maaptanao yaliafikiwa tena katika miaka ya 1980 baada ya Israel na Misri saini mkataba wa amani mwaka 1979.
Hatima ya wengine elfu tisa ambao bado wako Ethiopia inatarajiwa kuangaziwa katika mazungumzo kati ya serikali hizo mbili baadaye Alhamisi. Licha ya hayo, nchi hizo mbili zinajivunia kuwa washirika wa karibu katika vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi na kuwa na msaada wa Marekani. Ziara pia anatarajiwa kuendeleza mahusiano baina ya nchi hasa katika maeneo ya biashara, usalama, kilimo na elimu.
No comments
+255716829257