MUUAJI WA WATU WATATU MSIKITINI JIJINI MWANZA ATOROKA MIKONONI MWA POLISI..

Kamanda wa
polisi wa mkoa huo, Ahmed Msangi alisema juzi mtuhumiwa huyo ambaye ni
mkazi wa Nyegezi, alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka walipojificha
wenzake katika mlima Kiloleli Nyasaka kata ya Kirumba wilayani Ilemela.
Msangi
alisema baada ya polisi na mtuhumiwa huyo wa ujambazi kufika eneo la
tukio saa 8:00 usiku ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima
huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu
mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka ndipo alipopata mwanya wa kutoroka.
Aidha
alisema katika mapigano hayo, polisi walikamata bunduki aina ya shortgun
iliyokatwa mtutu na kitako na risasi moja kwenye chemba iliyotupwa na
majambazi hao.
No comments
+255716829257