FID Q: JE NI MUZIKI GANI WAKUPAMBANA NA UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI??..

Rapper Fid Q a.k.a Ngosha na gwiji wa muziki wa Hip hop Tanzania amefunguka ya moyoni jinsi muziki wa Tanzania kwa namna moja ama nyingine huweza kutoa maudhui yenye kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii husika ikiwemo maadui wakubwa wa maendeleo ambao ni UJINGA, UMASIKINI na MARADHI.
Akiongea na kipindi cha LADHA 3600 cha Efm kinachoongozwa na mtangazaji, Kibonge TOZ, amesema kuwa muziki wa Hip hop ndio mziki pekee unaotoa mafunzo mbalimbali yenayoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za mtanzania kutokana na aina ya ujumbe unaopatikana katika nyimbo hizo ikilinganishwa na aina nyingine za muziki wa kizazi kipya ambazo hutoa maudhui ya kimapenzi zaidi.
Amesema muziki wa Hip hop una nafasi kubwa sana katika jamii ya kitanzania na hata unapopigwa kwenye showz mbalimbali unaonekana kuamsha hisia za mashibiki kuliko aina nyingine za muziki.
Aidha Fid ameongeza kuwa ipo tofauti kubwa kati ya muziki wa Hip hop na TRAP, ambayo ni aina ya muziki inayofanana na Hip Hop ikizingatiwa kuwa aina hiyo ya muziki pia ni yakufokafoka ambayo inaonekana kuovertake Hip Hop halisi na rappers wengi wa Tanzania na dunia hujikuta wakibadilika kufuata mtindo huo, kitendo Fid Q anachoonekana kukipinga vikali.
Fid Q ameihusisha sanaa ya muziki na falisafa ya Mwalimu J.k Nyrere ya kupambana na maadui watatu wa maendeleo, UJINGA, UMASIKINI na MARADHI.
No comments
+255716829257