UTAFITI: ASILIMIA 87% YA WATANZANIA NI WALEVI, KILIMANJARO NA DAR ES SALAAM WANAONGOZA.
Utafiti uliofanywa na shirika la Afya Dunia ‘WHO’ umeonesha kuwa 87% ya watanzania wanakunywa pombe za kienyeji, huku mikoa ya Dar es salaam na Kilimanjaro ikiiongoza kwa kuwa na wanywaji wengi wa pombe hiyo.
Mkoani
Kilimanjaro eneo linaloongoza kwa wanywaji wa pombe hiyo ni Moshi, kwa
mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania ilikuwa na watu
wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 44.9, hivyo 87% ya idadi hiyo
kulingana na utafiti huo ni watu milioni 39.06.
Kulingana na gazeti la Jambo Leo
limeeleza kuwa utafiti huo umebaini kuwa kwa sasa vijana wengi
wanatumia pombe kupita kiasi kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu
hali inayosababisha wakumbwe na magonjwa ya akili na kujiingiza kwenye
vitendo vya uhalifu.
Matokeo ya
utafiti huo yalitangazwa jana katibu mkuu wa chama cha wataalam wa afya
ya akili Tanzania (MEHATA), Dk. Kissah Mwambene. Alikuwa akitoa mada
kwa wabunge juu ya athari za matumizi za matumizi ya pombe iliyoandaliwa
na chama cha waandishi wa habari wanawwake ‘TAMWA’.
No comments
+255716829257