SOMALIA: MLIPUKO MKUBWA WALIPUKA KATIKA HOTELI MJINI MOGADISHU..
Mlipuko mkubwa umekumba hoteli moja
katikati ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kuna sauti za ufyatulianaji
wa risasi katika kile kinachoaminika huenda ni shambulio la wapiganaji
wa al-Shabab.
Kulingana na mwandishi wa BBC Ibrahim Aden mjini
Mogadishu, mlipuko huo ulikumba hoteli ya Naso Hablod ikiwa ni hatua
chache kutoka kwa uwanja wa ndegewa mji huo.Hakuna ripoti zozote za majeruhi.
Ripoti zinasema kuwa huenda kulikuwa na mlipuko wa pili
Wapiganaji wa al-Shabab hutekeleza mashambulio ya mara kwa mara katika mji huo kwa lengo la kuiangusha serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.
''Walianza na mlipuaji wa kujitolea muhanga na baadaye kuvamia.Kwa sasa wako ndani na ufyatuliaji mkubwa wa risasi unaendelea'' ,alisema msemaji wa polisi meja Nur Farah.
chanzo: BBC
No comments
+255716829257