Habari mpya

RAPPER YOUNG DEE AKIRI KUWA ALIKUWA AKITUMIA MADAWA YA KULEVYA..

 
Rapper Young Dee amesema alikuwa akitumia madawa kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu licha ya kuzipinga tuhuma hizo mara kwa mara alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari mara kadhaa.
Akiongea na Fresh news ya ladha 3600 ya Efm, Rapper huyo aliyewahi kutamba na vibao kama teacher, tunapeta, dada kaolewa, kijukuu, Ujanja ujanja na nyingine nyingi amesema kuwa alijikuta akiingia katika mkumbo huo wa matumizi ya dawa za kulevya kutokana na ushawishi wa marafiki, hata hivyo Young Dee amekiri kuacha matumizi hayo yanayomfanya kujutia maamuzi yake anayoamini yalimrudisha nyuma kimuziki.
Aidha Young Dee ameongeza kuwa kwa sasa amerudi katika management yake ya zamani ya MDB ambako anatarajia kuendelea kufanya vizuri zaidi kimuziki.

Kumekuwa na wimbi kubwa la matumizi ya madawa hatari ya kulevya miongoni mwa wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya.

No comments

+255716829257