Habari mpya

Mabaki yanayokisiwa kuwa ya ndege ya Malaysia yapatikana TZ..

Maafisa wa uchukuzi wanachunguza iwapo mabaki ya ndege yaliyopatikana ufuoni ni ya ndege ya Malaysia iliyotoweka miaka miwili iliyopita.
Picha za mabaki hayo yaliyopatikana visiwa vya Pemba zimekuwa zikisambaa sana mtandaoni.

Maafisa wa Tanzania wamewasiliana na maafisa wa Malaysia ambao wanapanga kutuma wachunguzi,
Hilo litawezekana tu wakati watengenezaji wa ndege hiyo watafika na kuchunguza mabaki hayo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uchukuzi wa Ndege Tanzania Redemptus Bugomola ameambia BBC kwamba bado ni mapema mno kubaini iwapo mabaki hayo ni ya ndege ya MH370.
Shirika la habari nchini Malaysia Bernama lilimnukuu waziri uchukuzi nchini humo Liow Tiong Lai, akisema kuwa mabaki ya ndege hiyo yatafanyiwa uchunguzi kubainia ikiwa yana uhusiano na ndege ya Malaysia iliyopotea ya MH370.

"Mabaki hayo ya ndege ni makubwa ... lakini ni baada tu ya kubaini kwamba ni ya ndege aina ya Boeing 777 ndipo tutatuma wachunguzi huko kwenda kuchunguza iwapo kweli ni ya MH370 au la," amesema Liow.
Ndege hiyo ya Boeing 777 nambari MH370 ilitoweka 2014 ikiwa na watu 239 muda mfupi baada ya kupaa kutoka Kuala Lumpur ikielekea Beijing.

Vipande vya ndege hiyo vilipatikana katika visiwa vya Reunion Julai mwaka 2015.
Hivi majuzi, mabaki ya ndege sawa na hiyo yalipatikana Madagascar lakini baada ya uchunguzi ikabainishwa kwamba hayakuwa ya ndege hiyo ya MH370.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257