JIFUNZE HAPA KILIMO BORA CHA TANGAWIZI..
Kwa ujumla tangawiz hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800
mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na
tangawiz zinastawi.
KUANDAA SHAMBA
Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya
April, may au June, ni vizuri
ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha
udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.
KUPANDA
KUPANDA
Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha
mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45
mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia mbolea ya mboji au
samadi na usitumie mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz
hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25
inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz. Huchukua
wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na
joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na
gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda.
Palilia Mara Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili
tangawiz itanuke vizuri.
MAGONJWA
Tangawizi haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa
na kuvu (fungus).
KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko
toka usawa wa bahar na mvua.
Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya
mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya
tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka
Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini
kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa
hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport,
wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani
Uzuri tangawiz unaweza kusubir soko zuri na ukauza kwa bei
nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka
Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa
kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa
kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzà lisha mbegu ambazo
utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata
uzoefu kupitia hapo na kujua kama eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa
kilimo cha tangawizi.
HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la
wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na
udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.
Matikiti hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya
21-30 sentigradi. Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini
ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota
Mvua: kwa upande wa mvua matikiti
yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi
husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile
vile haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali
kubwa. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo
vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0.
credit: miradi kwanza.
No comments
+255716829257