India: Aliyeongoza katika mtihani afungwa jela kwa udanganyifu.
Hivi ndivyo ulivyo udanganyifu katika mtihani India.
Mwanafunzi mmoja wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili.
Ruby
Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo
katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo
la sayansi ya siasa linahusu mapishi.Baada ya kanda hiyo kusambaa ,bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali.
Aliwasilishwa mahakamani siku ya Jumapili ambapo hakimu alimuhukumu kifungo jela hadi tarehe 8 mwezi Julai.
Uamuzi wa kumpeleka jela umekosolewa kwa kuwa ni mtoto na kwamba badala yake angepelekwa katika jela ya watoto.
chanzo: BBC
No comments
+255716829257