Habari mpya

DULLAYO ASEMA MUZIKI HAUJABADILIKA SANA..

 
Mwanamuziki wa kizazi kipya Dullayo aliyewahi kutamba na hits kali kama naumia roho, bila yule, mida ya kazi, twende na mimi na nyingine nyingi ameibuka na kusema muziki wa  sasa hauna jipya lolote licha ya wasanini wengi kuamini kuwa kufanya vizuri katika muziki unaofanyika sasa hivi msanii hana budi kubadilika sana kama ambavyo tunweza kujionea wasanii wengi wakibadilika kutokana na soko.
Akiongea katika kipindi cha ladha 3600 cha Efm, Dullayo amesema kuwa muziki haujabadilika sana kulinganisha na wa zamani zaidi sana muziki wa sasa umekuwa ukichuja haraka sana mithili ya ladha ya peremende hivyo kuwalazimu wasanii kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja kuhofia kupotea kwenye game.
Aidha hit maker huyo wa WALEO, ameongeza kuwa mpaka hivi leo bado anapata show nyingi kupitia nyimbo zake kudhihirisha kuwa mziki wa zamani ulikuwa unaishi kwa muda mrefu.

Dullayo bado ana kimya cha muda mrefu bila kutoa wimbo wowote uliofanya vizuri siku za karibuni.

No comments

+255716829257