CHILE WASHINDI WA COPA AMERICA 2016..
Michuano ya Copa America imefikia
tamati huku mabingwa watetezi Chile kuendeleza ubabe wake dhidi
ya Vigogo wa soka duniani Argentina.
Dakika 120 za mchezo huo
zilishuhudia timu hizo zikienda suluhu ya bila kufungana. Mchezo huo
ulitawaliwa na ubabe wa hapa na pale huku ikushuhudiwa timu zote mbili
zikimaliza kipindi cha kwanza zikiwa na wachezaji 10 baada ya Marcelo
Diaz wa Chile kulambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu dakika ya 28
kabla ya Marcos Rojo wa Argentina kutolewa nje dakika ya 43 kwa kadi
nyekundu ya moja kwa moja. Katika upigaji wa penalti,Arturo Vidal wa
Chile alianza kwa kukosa kabla ya Lionel Messi na Lucas Biglia kukosa
kwa upande wa Argentina. Hii inakuwa fainali ya pili ndani ya miaka
miwili kwa timu hizi mbili kukutana katika hatua ya fainali amapo mara
zote mbili Chile wamechukuwa kikombe hicho kwa mikwaju ya penalti.
Fainali hizi zilichezwa mwaka jana nchini Chile na kurudiwa mwaka huu
ikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 tokea kuanza kwa michuano hii mwaka
1916.
No comments
+255716829257