Habari mpya

ALIYEMTUKANA RAISI MAGUFULI HATIANI.

 Image result for whatsapp
Mulokozi Kyaruzi amefunguliwa mashtaka kutokana na ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo anadaiwa kumtusi Rais John Pombe Magufuli.
Kyaruzi ameshtakiwa chini sheria ya uhalifu wa mtandaoni.
Ni mtu wa pili kushtakiwa chini ya sheria hiyo kwa tuhuma za kumtusi rais.
Sheria hiyo inakosolewa sana kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza wakati ilipoanza kutekelezwa mwaka uliopta.
Kyaruzi anadaiwa kuandika: "'Kwani rais Magufuli hana washauri? hashauriki? Ama ni mjinga tu? Ni Mpumbavu sana. Haangalii sheria iliopo kabla ya kufungua mdomo ama anaugua ugonjwa wa Mnyika''?.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257