Habari mpya

Yanga na Tp Mazembe kundi moja

Image captionTp Mazembe
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho klabu ya soka ya Yanga imepangwa kundi moja na timu ya Tp Mazembe.
Hatua hii ya nane bora imegawanywa katika makundi mawili yenye timu nne kila kundi ambapo kundi A kuna timu za Yanga ya Tanzania ,Tp Mazembe ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo,Mo Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Huku Kundi B likiwa na timu mbili za kutoka nchini Morocco ambazo ni Kawkab na Fus Rabat na pia kuna Etoile du Sahel ya Tunisia na Ahly Tripoli kutoka nchini Libya.
Mechi za Kwanza za makundi kwa zitachezwa kati ya Juni 17 na 19, na za Pili ni kati ya Juni 28 na 29,mechi za Makundi zitamalizika tarehe 23 na 24 Agosti na washindi wawili wa kila kundi kutinga nusu fainali.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257