Wavalia vyuma katika tamasha la Met
Watu maarufu katika tamasha la sanaa ya makumbusho mjini New York walivalia mavazi ya vyuma huku wakisheherekea mkutano wa binadamu na Mashine.
Hatahivyo sio wote waliohudhuria tamasha hilo walivaa kulingana na madhari ya tamasha hilo.
Tamasha hilo la kila mwaka huiletea mamilioni ya fedha taasisi ya nguo za makavazi.
Mwaka uliopita wale waliohudhuria tamasha hilo walitakiwa kuvaa kulingana na mandhari ya ushawishi wa China katika fesheni za kimagharibi na kulikuwa na ufanisi mkubwa.
Mwaka huu mandhari ya maonyesho hayo ni Manus x Machina: Fesheni katika miaka ya Teknolojia.
Tiketi mwaka huu ziliuzwa kwa dola 30,000 kwa mtu mmoja,lakini licha ya bei hizo za tiketi ni sherehe ambayo ni vigumu kuhudhuria.
Faragha ya wageni hulindwa sana,na uchapishaji wa mitandao ya kijamii baada ya kuingia katika zulia jekundu umepigwa marufuku tangu mwaka jana.
Mwaka uliopita zaidi ya dola milioni 12 zilichangishwa katika taasisi hiyo ya mavazi ya makavazi.
source: BBC
No comments
+255716829257