Habari mpya

Ukame: Burkina Faso kutoa maji kwa mgao

Image copyrightThinkstock
Image captionUkosefu wa maji ulishuhidiwa mwisho mwaka 2013 hata hivyo hali imekuwa mbaya kwa sababu ya kiangazi.
Burkina Fao itaanza ugavi wa maji katika mji mkuu Ouagadougou, kutokana na ukosefu mkubwa wa maji.
Waziri mmoja alisema kuwa serikali imeamua kufunga maji kwenda wilaya tofauti za mji baada ya kila saa 12.
Wiki chache zilizopita baadhi ya maeneo ya Ouagadougou yamebaki bila maji kwa siku kadhaa.
Image copyrightAFP
Image captionBurkina Faso kutoa maji kwa mgao
Ukosefu wa maji ulishuhidiwa mwisho mwaka 2013 hata hivyo hali imekuwa mbaya kwa sababu ya kiangazi.
Hatua hizo mpya zitaanza kutekelezwa siku ya Jumanne juma lijalo.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257