Uhuru ataka mmiliki wa jumba la maafa kukamatwa
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaka kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba ilioanguka mjini Nairobi na kuwaua watu saba.
Kenyatta aliyezuru mkasa wa tukio hilo pia amewataka wakaazi wa nyumba zilizopo karibu na eneo hilo kuondoka wa kuwa nyumba hizo zimethibitishwa kutokuwa salama.
Maafisa wa Kaunti ya Nairobi wamethbitisha kuwa nyumba hiyo ilikuwa imeorodheshwa miongoni mwa majumba yaliotarajiwa kuvunjwa kwa kuwa haikuafikia viwango vya nyumba ya kuishi watu wengi.
Juhudi za uokoaji zinaendelea lakini zimetatizwa na mvua kubwa inayoendelea mbali na uwezo wa kufikia eneo hilo.
Jeshi la Kenya linaloongoza juhudi hizo za uokozi limelazimika kutumia mikono na misumeno ya kielektroniki kuchimba chini ya vifusi kwa kuwa vifaa vinavyohitajika katika zoezi hilo haviwezi kuingia katika eneo hilo.
source: BBC
No comments
+255716829257