Habari mpya

Simba waliotekwa Peru watua Afrika Kusini

Image copyrightAP
Image captionSimba waliotekwa Peru watua Afrika Kusini
Simba 30 waliookolewa nchini Peru na Colombia wamewasili nchini Afrika Kusini baada ya kusafirishwa kwa ndege na shirika la kupigania haki za wanyama.
Waandishi wa habari walisema kuwa simba hao walionekana wenye afya licha ya kuchoka kufuatia safari ndefu kutoka Amerika ya Kusini.
Image copyrightAP
Image captionBadhi yao meno na makucha yao yameng'olewa na itakuwa vigumu wao kuishi mbugani.
Kundi hilo ambalo walipigania kubadilishwa kwa sheria na kuharamisha wanyama kutumiwa katika utumbuizaji na sarakasi.
Simba hao watapelekwa eneo moja la kuwatunza Kaskazini mwa Afrika Kusini ambapo wataishi maisha yao yote.
Image copyrightAFP
Image captionSimba hao watapelekwa eneo moja la kuwatunza Kaskazini mwa Afrika Kusini
Badhi yao meno na makucha yao yameng'olewa na itakuwa vigumu wao kuishi mbugani.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257