Habari mpya

SHILOLE KAFUNGUKA HAYA BAADA YA WIMBO WA SNURA KUFUNGIWA..

Ni Mei 4, 2016 ambapo kupitia wizara ya Habari na Utamaduni, Michezo walitoa taarifa za kuufungia wimbo wa Snura ‘chura’ kuchezwa kuanzia leo na kuitoa nyimbo hiyo kwenye mitandao yote ya kijamii mpaka hapo Snura atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo. 
Sasa taarifa hizo zimemfikia Soudy Brown wa U Heard wa kipindi cha XXL ambapo kwenye Uheard amesikika Snura alichowahi kuzungumza kabla ya ngoma yake kufungiwa…..
>>>siruhusu video yangu kuchezwa kwenye TV yoyote, ile video ni ya youtube kwa hiyo mtu anaposema maadili, sijui watoto, huyo mtoto anayeacha kwenda library kujisomea na kutafuta chura youtube huyo ni mtu mzima’:
Soudy Brown amezungumza na Shilole na kumuuliza kama amesikia wimbo wa ‘Chura’ kufungiwa, Shilole amezungumza machache katika sauti ifuatayo...
Sauti ya mahojiano ya Sudy Brown, SNURA na SHILOLE fuata link hii...http://www.hulkshare.com/millardayo1/u-heard-may-04-1
chanzo: millardayo.com

No comments

+255716829257