Habari mpya

Ranieri awataka nyota wake kusalia

Image copyrightAP
Image captionRanieri
Meneja wa kilabu ya leicester Claudio Ranieri amewataka nyota wake katika kikosi chake kusalia katika timu hiyo kwa mwaka mmoja zaidi.
Mbweha hao waliwashangaza wengi kwa kushinda ligi hiyo baada ya kutumia pauni milioni 57 pekee msimu huu.
Ni miujiza mkubwa! Tungependa kusalia katika ligi kuu ya EPL msimu ujao''
Aiyawatt Srivaddhanaprabha, naibu mwenyekiti Leicester
BBC
Winga Riyad Mahrez ,mshambuliaji Jamie Vardy na kiungo wa kati N'golo Kante ni miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo wanaotarajiwa kuondoka na kujiunga na timu nyengine msimu ujao.
''Nina matumaini tele'',alisema Ranieri.''Musiende''.
Image copyrightGetty
Image captionNyota wa Leicester
''Mukienda timu nyengine huenda musishirikishwe katika mechi''.
Wahandishi wa habari walimpatia heshima kwa kusimama kocha huyo wa Itali aliyechukua mahala pake Nigel Pearson msimu uliopita wakati alipowasili kwa mkutano na vyombo vya habari.

No comments

+255716829257