Habari mpya

RAIS MAGUFULI ASEMA VIJANA NDIO WACHAPAKAZI SERIKALINI..


Miongoni mwa stori kubwa ni hii ya gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Magufuli kujaza vijana Serikalini‘ Gazeti hili limeripoti kuwa Magufuli amesema kuanzia sasa wateule wengi wa Serikali watakuwa vijana kwa kuwa amegundua wengi hawapendi rushwa.
Gazeti hilo limeongeza kauli ya Rais Magufuli kuwa anafahamu kwamba vijana hawapendwi lakini amegundua ndio wachapakazi ambao watasaidia kulipeleka Taifa katika maendeleo anayoyatamani kwani aliowaweka tayari ameshaanza kuona matunda ya kazi zao.
Rais Magufuli aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa makandarasi wa mikoa ya Dar es salaa, Mbeya na Dodoma.

kutoka: millardayo.com 

No comments

+255716829257