Habari mpya

Mwanasesere wa ngono adhaniwa kuwa malaika

Image captionMwanaserere wa ngono
Maafisa wa polisi nchini Indonesia wamekipokonya kijiji kimoja mwanasesere anayetumika kufanyia tendo la ngono baada ya wakaazi wa eneo hilo kudhania kwamba alikuwa malaika.
Mwanasesere huyo mwenye maumbile ya kike alipatikana na mvuvi mmoja akiolea baharini mnamo mwezi Machi katika kisiwa cha Banggai mkoani Sulawesi.
Familia yake ilimchukua na mda mfupi baadaye picha zikaanza kuenea katika mitandao ya kijamii pamoja na madai kwamba alikuwa malaika.
Maafisa wa polisi walichunguza kisa hicho kufuatia hofu kwamba uvumi huo huenda ukasababisha machafuko kabla ya kubaini kwamba ni mwanasesere anayejazwa upepo na baadaye kutumiwa kingono.
Chombo cha habari cha Indonesia Detik kilisema kuwa picha za mwanasesere huyo akiwa amevalia hijab zilianza kusambaa katika vyombo vya habari baada ya kupatikana.
Uvumi ulianza kwamba alikuwa 'bidadari' pamoja na habari nyengine kwamba alipatikana amekwama akilia na kusababisha uchunguzi wa polisi.
Image captionMwanaserere Indonesia
Watu wengi hususan nchini Indonesia wanaamini uwepo wa bidadari ambaye ni malaika.
Afisa mkuu wa polisi Heru Pramukarno aliiwambia wanahabari kwamba wana vijiji walimpata mwanaserere huyo baada ya jua kupatwa na mwezi .
Kupatikana kwake kuliwafanya wengi kuamini kwamba alikuwa na nguvu fulani.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257